Roho ya Korosho


Ewe Mheshimiwa unayebubujika vitisho,

Laiti ningelijua una roho ya korosho:

Roho ngumu kama lilolelewa kwenye mkorosho,

Roho mbaya lilojikunja mithali ya korosho…

 

Walahi, ningekutia kwenye karai la kukaanga

Nikakukoroga chumvini kiuganga

Kisha nikakuhifadhi kwenye mkoba wangu wa karanga.

 

Jumamosi, ningekubeba mfukoni hadi ugani Kasarani,

Na pindi kipenga kianzishapo kabumbu uwanjani,

Ningeshabikia kukutafuna roho: korosho baada ya korosho

Huku nikiyasaga vyako vitisho kwa mara ya mwisho!

© OLUOCH-MADIANG’.

Advertisements

4 responses to this post.

 1. Posted by Jahazi on September 15, 2011 at 18:58

  Ustaaz Malenga Madiang’….Diwani ya Alego.

  Reply

 2. Posted by Peter on September 15, 2011 at 21:52

  Shairi la hali ya juu. Sikujua wewe ni mshairi…malenga. Wacha nisome mashairi mengine. Kazi nzuri hii.
  Amunga

  Reply

 3. Reading the poem reminds me of days in primary and high school when learning Visawe, now I need to get the different meanings of these words.

  Reply

 4. Posted by marcus on September 29, 2011 at 16:27

  Hongera!! chunga sije nyongwa na vitisho vya mashua kwani roho ya korosho halishitui bahari.

  Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: