ETI WEWE SIMBA?


Kila mtu na mtuwe swahiba!

Simba ndiye mkali porini
Simba ndiye aogopwae mwituni.
Yeye auae watu akawala –
Auae wanyama wenza akawala.

Lakini hata naye na ukali wake
Lakini hata naye kwa ukali wake
Hutulizwa.
Huliwazwa.
Hubembelezwa.
Akajilaza tani kwa hiari yake yeye mwenyewe
Hadi akaumbishwa Simba mwana.

Yuyo huyo Simba mkali, atishae wote porini.
Yuyo huyo Simba mla watu, mfalme wa mwituni.

Eti wewe Simba?
Usinitanie swahibu: kila Simba ana simbawe!

© OLUOCH-MADIANG’

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: